Skip to main content

Successful Event: TAMASHA LA VIJANA 10 DEC 2016

25
0

Muhubiri 12:1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo."

Ni tamasha liliondaliwa na Akuzamu Youth of Love Mahususi Kwaajili ya Kuwakutanisha vijana wote kutoka Madhehebu MbaliMbali ili kumsifu na kumwabudu Mungu pamoja huku wakidhihirisha vipawa mbalimbali walivyojaaliwa na Bwana. Pia Hii ni nafasi nzuri kwa vijana kufahamiana kama ndugu katika KRISTO, Kushirikishana changamoto mbalimbali za Ujana na namna ambavyo tunaweza kuzishinda ili Tuwe waaminifu kumtumikia Mungu siku za Ujana wetu kabla hazijaja siku zile Mbaya. Vijana tuna changamoto nyingi sana katika Maisha haya ya Ujana lakini Mungu anapendezwa sana Tukimtumikia katika Ujana wetu hivyo Basi hatuwezi Kulitimiza Hili kusudi isipokuwa kwa kujitoa kwa nguvu zetu katika kumsifu na kumwabudu Mungu.
kama siku zile za Paulo na Sila katika taabu yao walimsifu Mungu na Mungu akashughulika na Hitaji lao. USIPANGE KUKOSA TAMASHA HILI LA KIHISTORIA VIKUNDI MBALIMBALI na WAIMBAJI BINAFSI WATAKUWEPO kama vile ATOSHA KISSAVA , the bridge to the next level, R.I.O.T SQUAD (wazee wa t-shirt na jeans), akuzamu youth of love, Rungu la Yesu, Fire, PETER BANZI na wengine mbalimbali, MWALIKE NA MWENZAKO HAKUNA KIINGILIO.ubarikiwe

admin