Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | UNAPASWA KUJILINDA SANA, KWA SABABU UNAWINDWA SANA ( UJUMBE KWA VIJANA WA KANISA LA LEO)

23
0

Niliokoka nikiwa na umri wa miaka 19, nilikuwa bado kijana mdogo kiumri hata ki-umbo!.

 

Siku moja usiku nilipokuwa nimelala Roho Mtakatifu alisema na mimi kwa sauti ya upole sana, aliniambia "JILINDE SANA, UNAWINDWA SANA",

Nilipoamka tu nikaanza kutafakari ile sauti, nikajiuliza sana maswali,

 

Nilianza kwa kujiuliza, "NIWINDWE MIMI NINA NINI?"

 

Huku nikijiangalia umbo langu, nikaendelea kujiuliza tena "MBONA UMRI WANGU BADO MDOGO?, MBONA SINA HELA?, KWA NINI NIWINDWE?"

 

Nilijiuliza maswali hayo yote, kwa sababu nilikuwa nataka KUJUA sababu ya mimi KUWINDWA SANA!

 

 Na kusema kweli wakati huo kulikuwa na maneno maneno mengi tu yaliyokuwa yanainuka kwa ajili yangu, tena mengine yalikuwa yanasemwa na watu walionizidi sana kiumri, pia ni watu niliowakuta Kanisani!.

 

Ikabidi Roho Mtakatifu anisaidie tena, kwa kunipa sababu za 'KUWINDWA KWANGU'

 

(Kuna vitu alinisemesha ili kunijibu maswali yangu).

 

Leo nimejikuta natafakari kuhusu huu ushuhuda, alafu nikasukumwa sana KUKULETEA UJUMBE KWAMBA "UNAPASWA KUJILINDA SANA, KWA SABABU UNAWINDWA SANA"

 

Biblia inasema "Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye ALIYEZALIWA NA MUNGU HUJILINDA, wala yule mwovu hamgusi."

1 Yohana 5 :18

 

ninalitaka Lile neno linasema 'BALI YEYE ALIYEZALIWA NA MUNGU, HUJILINDA'

 

Wewe UMEZALIWA NA MUNGU?

 

Kama wewe UMEOKOKA maana yake UMEZALIWA NA MUNGU KWA NENO LA KWELI; kama MAANDIKO yanenavyo!.

 

Unapaswa KUJILINDA ili yule MWOVU ASIKUGUSE;

 

Unapaswa kujilinda ili YULE MWOVU ASIKURUDISHE NYUMA,

 

Unapaswa kujilinda ili yule MWOVU ASIKUIBIE YALIYOPANDWA NDANI YAKO!

 

Wewe ni ASKARI WA WEWE MWENYEWE, yaani namaanisha 'wewe ni MLINZI WAKO'

 

Wewe ni MGODI Wenye MADINI yasipatikana kwenye DUNIA hii,

MADINI hayo yanatakiwa YATUMIKE KWA MANUFAA YA UFALME WA MUNGU;

 

Adui asingependa IWE HIVYO, ndio sababu 'UNAWINDWA SANA'

 

Mungu anakwambia katika NENO lake kwa 'LINDA SANA MOYO WAKO; KULIKO YOTE UYALINDAYO' unajua kwa nini? Kwa sababu huko NDIKO YALIPO HAYO MADINI NA CHANZO CHA MADINI HAYO!

 

'Unawindwa sana'

 

Angalia VIPAWA VINGI VYA VIJANA VIMEFUKIWA NA KIFUSI KIITWACHO 'DINI'

 

Angalia, MAONO YA VIJANA WENGI YAMEFUKIWA NA KIFUSI KIITWACHO 'DHAMBI',

 

Wengine wameliwa na 'MAGONJWA YA AJABU'

 

Wengine WAMECHUKULIWA MATEKA NA 'MAPOKEO'

 

Ogopa sana MAONO/VIPAWA/HUDUMA/KARAMA kufukiwa KATIKA VIFUSI HIVYO!

 

Vijana wengine HUDUMA ZAO zilikutana na 'HERODE', Zilipoanza tu KUCHANUA; 'HERODE AKAZIKATA VICHWA',

 

Vingine VIMEWEKWA GEREZANI!

 

Ndio maana Nimekwambia wewe 'UNAWINDWA SANA'

 

Roho Mtakatifu ni mzuri sana, amekuona ANATAKA AKUSAIDIE KIJANA!.

 

Jilinde UNACHOKULA/UNACHOLISHWA,

 

Jilinde na UNACHOSIKIA na UNACHOTAZAMA; vingine vipo kwa ajili ya KUKUBOMOA JUMLA!

 

Jilinde na MANENO UNAYOYAZUNGUMZA, ILI UOKOE NAFSI YAKO!.

 

Jilinde na KILA AINA YA SANAMU,!.

 

UNAPOENDELEA NA UTUMISHI ULIOITIWA,

UNAPOENDELEA NA KAZI ZAKO ZA KILA SIKU,

UNAPOENDELEA NA HUDUMA, USISAHAU 'KUJILINDA' MWOVU ASIKUGUSE!!.

 

Bwana Yesu  sana!!.

 

Nimesukumwa sana nikukumbushe haya MACHACHE,

 

"UNAPASWA KUJILINDA SANA, UNAWINDWA SANA"

 

Na:  Mwl. Nickson Mabena

        (WhatsApp#) 0712265856

 

admin