Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | MITI ILIYOOTA KANDO YA BARABARA

15
0

Kama umewahi kusafiri utakuwa umewahi kuiona miti ya aina mbalimbali KANDO ya Barabara, miti mingine inafahamika kwa majina na miti mingine haifahamiki kabisa!

 

Utakuwa umewahi tu kuiona miti hiyo hata ikiwa HUJAWAHI KUSAFIRI.

 

Niizungumzie kidogo MITI ya MATUNDA iliyoota pembezoni mwa barabara za magari au treni,

 

Nisizungumzie miti hiyo tu, bali na MITI YA MATUNDA iliyoota kwenye mitaa mbalimbali bila ya kumjua aliyeipanda miti hiyo!.

 

Wasafiri wengi hununua vitu (VYAKULA) mbalimbali kwa ajili ya kula njiani wawapo kwenye safari, miongoni mwa vitu vinavyonunuliwa Sana na wasafiri ni MATUNDA; mfano, Maembe, Machungwa, Ndizi, Mafenesi n.k

 

Wasafiri hao wawapo njiani, hutoa MATUNDA hayo na kuanza kula, ni wazi kwamba mtu anayekula embe lazima atatupa KOKWA la embe kwa dirishani/chombo cha kuhifadhia taka kilichomo ndani ya Gari!

 

Vivyo hivyo  kwa mtu atakaye kuwa anakula machungwa atazitupa zile mbegu kwa dirishani.

 

Nimetafakari hivi;-

 

Kuna miti mingi imeota na ikawa mikubwa tu lakini HAKUNA ALIYEKUSUDIA KUIPANDA ili iote,

Imejiotea baada ya WASAFIRI KUTUPA MBEGU ZA MITI HIYO MADIRISHANI MWA MAGARI,

 

Mwenye MITI hiyo HAJULIKANI,

Aliyeipanda HAJULIKANI,

 

Ukitaka kumfahamu aliyeipanda hutampata kwa sababu alikuwa ni Msafiri mmoja aliyekuwa anatoka Kijiji cha Msijute kule Mtwara akielekea Jijini Dar, alipofika mnazi Nangulukulu akanunua Samaki wake pamoja na machungwa, akiwa anakula njiani akatupa mbengu baadaye ZIKAOTA ndio ikawa machungwa hiyo unayoiulizia, Je! Huyu MTU utampata wapi?

Watakuaminisha mwenyewe kwa kukuonyesha ALIYEKINUNUA KIPANDE CHA ARDHI hiyo!

 

Ijapokuwa MWENYE MITI hiyo HAJULIKANI, habari njema ni kwamba "MATUNDA YA MITI HIYO YANAWANUFAISHA WENGI"..

 

sio matunda tu, bali hata KUNI, VIVULI, MBAO, MAJANI n.k ni Faida kwa wengi.

 

WAKATI NINAWAZA HIVI, NIKAKUMBUKA;-

 

KUNA WATU WANAFANANA KABISA NA HAO WASAFIRI

 

Aisee, Kuna watu ambao wana WATOTO karibia kila MKOA, mbaya zaidi hao watoto HAWAWAJUI BABA ZAO pia hata WATU wanashindwa kuelewa ni WATOTO WA NANI (nani ni mmiliki wa watoto hao?).

 

Kwenye mikoa ambayo kuna MASHAMBA ya Miti,

Wale vijana wanaojihusisha na UPASUAJI wa mbao huwa wana VITUKO sana,

Wakienda kuweka KAMBI sehemu kwa ajili ya kupasua mbao, PIA wanafanya kazi ya KUWAPA KULALA NA WASICHANA WADOGO kisha wanaondoka zao (WAMETUPA MBEGU);

 

Watengeneza Barabara na Madereva vivyo hivyo hufanya hiyo kazi ya KUTUPA MBEGU kisha wanasepa!

 

Kipindi cha ujenzi wa barabara nyingi sana hapa Tanzania, Wasicana wengi HUTUPIWA MBEGU kisha hujikuta na MIMBA bila ya KUMJUA aliyehusika, na upandaji wa MBEGU hizo (ALISHASEPA BAADA YA TUKIO).

 

Si hao tu,

 

Kuna  baadhi ya WATUMISHI pia hufanya hivyo,

Wanazunguka maeneo mbalimbali kwa ajili ya Huduma, na wao 'HUTUPA MBEGU KWA WADADA'

Baada ya muda MTUMISHI ANAKUWA NA WATOTO MAENEO MENGI ndani na NJE YA NCHI wakati huohuo hakuna anayejua kama watoto hao ni MATOKEO ya MTUMISHI Kupita kwenye MITAA YAO!

 

Walimu wa Kwaya mnaoenda Kufundisha wanakwaya Ndani na Nje ya Nchi, kisha MNATUPIA MBEGU KWA WANAKWAYA WENU then MNASEPA mkawachukue WATOTO WENU MUWATUNZE

 

Watoto wengi wamekuwa kama 'MITI ILIYOOTA KANDO YA BARABARA' hawawajui BABA ZAO,

wengine wameaminishwa tu kwamba baba yako ni FULANI kumbe siye Baba yake MZAZI bali ni MTU ALIYELIMILIKI HILO SHAMBA LIKIWA NA MBEGU TAYARI (sasa zimeota).

 

Baba uliyewatelekeza WATOTO wako kwenye vijiji X na Y ukawachukue UWATUNZE ni watoto wako wale!.

 

Vitu vingine unatakiwa kutafakari kabla ya KUFANYA;

Mwanaume MMOJA unakuwa na WATOTO kumi tena KILA MTOTO NA MAMA YAKE KWELI?

 

Wababa mngekuwa na HOFU YA MUNGU Leo hii tusingekuwa na WATOTO WA NJE YA NDOA, WATOTO WA MITAANI na WATOTO WASIOWATAMBUA BABA ZAO!

 

Baba; WALE WATOTO WANAKULILIA WEWE, USIJIKAUSHE MJINI bila kuwapa HUDUMA watoto wako wengine KISA unalinda NDOA yao!

 

Wale ni WATOTO wako pia WANA HAKI YA KUWA WARITHI KWENYE MALI ZAKO, na wao ni SEHEMU YA FAMILIA YAKO!

 

usiwafanye WATOTO wawe kama "MITI ILIYOOTA KANDO YA BARABARA".

 

Nimalizie kwa kukwambia hivi wewe MTOTO WA NJE YA NDOA, ULIYETUPWA NA BABA, ULIYEKATALIWA NA BABA, USIYEMFAHAMU BABA YAKO,  UNAYEWATAFUTA WAZAZI kwamba,

 

" MTI ULIOJIOTEA KANDO YA BARABARA, BADO UNA UWEZO WA KUZAA MATUNDA NA KUWANUFAISHA WENGI; WEWE BADO NI MTU MUHIMU SANA KATIKA UKIMWENGU HUU, TUNAYAHITAJI MATUNDA YAKO".

 

Nimemaliza

 

Na: Mwl. Nickson Mabena

       (Whatsapp#) 0712265856

 

admin