Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | KOSA WANALOLIFANYA WAZAZI WENGI!...

9
0

"Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakua katika moyo wako; NAWE UWAFUNDISHE WATOTO WAKO KWA BIDII, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo". KUMBUKUMBU 6:6-7 Bwana Yesu asifiwe, karibu kwenye Mfululizo wa Masomo haya Maalumu kwa ajili ya Kuongeza Wasomaji wa Biblia, Leo Mungu ameruhusu niutoe ujumbe huu kwa Ajili ya Wazazi, na walezi pia!. Siandiki ujumbe huu kwa lengo la kuwalaumu wazazi na walezi, bali kichwa cha ujumbe kilikuja hivyohivyo ndani yangu, na nimeshindwa kukibadilisha!. Ukisoma Biblia, Mungu alipokua anaongea na Wana wa Israeli, aliwasisitiza Sana kile anachowaambia, awaambie na Watoto wao, Mimi nilishangaa sana, anawabia kwanza wayashike wao, alafu na Wawafundishe watoto wao. Angalia kwenye sura hii ya Sita ya Kitabu cha Kumbukumbu la Torati, KUMBUKUMBU 6 1 Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; 2 upate kumcha BWANA, Mungu wako, kuzishika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na MWANAO, na mwana wa mwanao, siku zote za Maisha yako; tena siku zako ziongezwe. Mungu amesisitiza sana, kile wanachofundishwa na Mungu, wawafundishe na watoto wao!. Kutokana na Somo langu, nataka nikukumbushe Mzazi au mlezi, Kumnunulia Biblia huyo unayemlea!. Nikwambie kitu kimoja, Nilikua natafakari, jinsi Mzazi/Mlezi unavyomnunulia Mtoto wako Vifaa vya Shule, unamnunulia Begi, Counterbooks, Mkebe, Viatu, Uniform, n.k, Kwa Kifupi, anamnunulia vitu vyote vilivyoagizwa kwenye Joining Instructions, Lakini CHA AJABU, HUMNUNULII BIBLIA YA BEI RAHISI TU, Unasubiri wapewe vi agano jipya vya msaada mashuleni. Au kama ulimpeleka shule ya KiKristo, ambayo mtoto hawezi kusajiliwa, hadi awe Biblia (Zipo shule baadhi, zenye maelekezo hayo), Sasa, umempeleka Mwanao Shule, ajue Kusoma, Ameshajua, unataka Asome nini!?, Mwisho wake, atasoma visivyotakiwa kusoma!!. Kosa lako, ni KUSHINDWA KUMNUNULIA BIBLIA MWANAO, Nimefanya Huduma Mashuleni kwa Wanafunzi, Zaidi ya robo tatu ya Wanafunzi hawana Biblia, hii ni HATARI ZAIDI!. Utakuta Wamevaa Sare, Wamependeza, lakini hawana BIBLIA!. Binafsi inaniuma sana, shetani ametuchezea sana kwenye hili! Unajua Madhara yake ni nini!?. Madhara yake yapo hapa!. WAAMUZI 2, 10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; KIKAINUKA KIZAZI KINGINE NYUMA YAO, AMBACHO HAKIKUMJUA BWANA, WALA HAWAKUIJUA HIYO KAZI AMBAYO ALIKUA AMEITENDA KWA AJILI YA ISRAELI. 11 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa maovu mbele za macho ya BWANA, nao wakawatumikia mabaali 12 Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakafuata mingu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha BWANA, akaghadhibika. Madhara ndio hayo Kinainuka Kizazi, Kisichomjua Bwana!. Mimi nakushauri, Mnunulie Mwanao Biblia yake Mwenyewe!. Mfundishe Jinsi ya Kuisoma, Cha ajabu ni Kwamba, Wewe Mwenyewe, Husomi, ndio Maana huoni Umuhimu wa Mwanao kuwa na Biblia!!. Unamnunulia mwanao simu ili awasiliane na wewe, lakini hujamnunulia Biblia ili awasiliane na Mungu, huoni ajabu!? KOSA WANALOLIFANYA WAZAZI WENGI, HAWAWANUNULII WATOTO WAO BIBLIA, Mwaka huu, Usifanye Kosa hilo Tena, Mnunulie Mtoto Biblia, Mfundishe Kuisoma, na aisome TUMFILISI SHETANI 2016!. Barikiwa kwa kuusoma Ujumbe huu, Waambie na Wazazi wengine!!. Ahsante kwa Kunisikiliza!.

MWL. NICKSON MABENA

 

admin