Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | KAMA 'HAJATAHIRIWA' HATUMPI MKE ( UJUMBE KWA VIJANA WA KANISA LA LEO)

29
0

Ujumbe wangu kwa vijana wa Kanisa la Leo, hasa vijana wanye ndoto za kuoa au kuolewa!. 

Ujumbe wangu unasema "KAMA 'HAJATAHIRIWA' HATUMPI MKE"

Kabla 'hujanirushia jiwe' kunipinga, soma kwanza ujumbe hadi mwisho ili ujue ni nini hasa ninachomaanisha!.

Mwezi wa nane mwaka huu 2017 mimi (Mwl. Nick) nilikuwa nasoma kitabu cha Mwanzo kama utaratibu wa kujifunza Biblia. 

Nilipofika kwenye sura ya 34 kuna kisa kimoja nilipokuwa ninakisoma, nikasikia ndani yangu kukuandikia UJUMBE HUU, 

Ishu ilikuwa hivi;- 

Kuna jamaa mmoja anaitwa Shekemu, alilala na Dina binti yake Yakobo aliyezaa na Lea ( akambikiri; ), 
Jamaa ghafla 'akamzimia sana' Dina akawa tayari KUMUOA kabisa awe MKE WAKE!, 

Mzee Yakobo aliposikia habari ya kubikiriwa kwa binti yake AKAKAUSHA TU (naona alikuwa anayasubiri MAJEMBE yake yaliyokuwa machungani)

"Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja" MWANZO 34:5

Watoto wa Yakobo walipozinyaka habari za kubikiriwa kwa Dada yao; 'WALIMAINDI' ile MBAYA, zaidi sana WALIMMAINDI JAMAA aliyefanya UNYAMA ULE! 

Biblia inasema; "Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka" MWANZO 34:7

Watoto wa Yakobo walikasirika sana; kwa sababu KITENDO KILE HAKIKUPASWA KUTOKEA KATIKA ISRAELI..

Kitendo cha LIJAMAA tu kulala na 'MWANADASHOST' WA KANISANI HAIPASWI KUTOKEA! 

Siku hizi Wanawali wenye sifa za Mariam (Mama wa Yesu) wanapungua tu MAKANISANI kwa sababu kuna wakina 'SHEKEMU' kibao tu WANAOTENDA UPUMBAVU NDANI YA KANISA; nasema hivi "HAIPASWI KUTOKEA". 

Je! Wewe UKISIKIA Shekemu ameshafanya yake kwa 'Binti Yakobo' unajisikiaje NDANI YAKO!? 

Na wewe Binti UNAKUBALIJE KIRAHISI RAHISI TU 'SHEKEMU' AJE ALALE JUU YAKO WAKATI HAJAKUOA? 

Mimi sijui Dina alikuwa 'mlaini' kwa kiasi gani, kwa sababu Biblia inasema 
"Shekemu, Maana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, AKAMWONA AKAMTWAA, AKALALA NAYE, AKAMBIKIRI" Mwanzo 34:2

Wala hakukuwa na 'process' ndafu sana!, 
Sasa simaanishi kwamba kukiwa na process ndefu ndio ukubali; 

Turudi kwenye point... 

Shekemu pamoja na kufanya huo UPUMBAVU, akakomaa AMUOE DINA kwani 'alikuwa amemzimia' si kidogo. 

Baba yake akapeleka proposal kwenye Familia ya Mzee Yakobo; 

Nayapenda sana MAJIBU YA WATOTO WA YAKOBO  NA MASHARTI WALIYOYATOA;- 

"Wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe umbu letu MTU ASIYETAHIRIWA; INGEKUWA AIBU KWETU" Mwanzo 34:14

Ni AIBU KUBWA kumpa MKE MTU 'ASIYETAHIRIWA'

Wakaongeza kusema AKITAHIRIWA basi MKE ATAPATA BILA SHAKA! 

Hivi ni kwa nini WATOTO WA YAKOBO walikataa KUMPA MKE MTU ASIYETAHIRIWA? 

Kuna 'SOMO' gani hapo kwa KANISA? 

Wewe BINTI ULIYEOKOKA kama KANISA hupaswi kabisa kabisa KUOLEWA NA MTU 'ASIYETAHIRIWA'

Mtu ASIYETAHIRIWA ni nani?

Ni Mtu ambaye hajaingia AGANO na Mungu wa Ibrahimu, 

Tohara ilikuwa ni Ishara ya Kuingia AGANO na Mungu wa IBRAHIMU
(Mwanzo 17:9-14); 

Mungu amesema "Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule ATATENGWA na WATU WAKE; AMELIVUNJA AGANO LANGU" Mwanzo 17:34

Sisi kwenye agano Jipya; tuna TOHARA ISIYOFANYWA KWA MIKONO! 

"Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala TOHARA siyo ile ya nje tu katika mwili; bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani na TOHARA ni ya moyo, katika roho, si katika andiko;.....". Warumi 2:29

TOHARA YA KRISTO

"Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili mwili wa nyama, KWA TOHARA YA KRISTO" Wakolosai 2:11

"Jitahirini kwa BWANA, mkaziondoe govi za mioyo yenu......" Yeremia 4:4

Kwa hiyo; Mtu ASIYETAHIRIWA ninaweza nikasema ni MTU ASIYE-OKOKA, 

Kama ni hivyo basi, MTU ALIYEOKOKA HAIPASWI KUPEWA MKE HUKU KWA WALIOOKOKA, 

Kwa hiyo, kama Hujaokoka na unataka MKE ALIYEOKOKA SHARTI NI HILI "OKOKA KWANZA (utahiriwe kwanza), LAKINI SIO KWA LENGO LA KUPATA MKE; BALI KWA LENGO LA KUPATA UZIMA WA MILELE NDANI YAKO"

Baada ya hapo, utakuwa ume-qualify kujitwalia MKE MIONGONI MWA "BINTI-YAKOBO". 

Aisee wewe BINTI ULIYEOKOKA; USIKUBALI KUTWALIWA NA JAMAA TU, AMBAYE HAJAINGIA AGANO NA MUNGU WAKO; 

Nisikilize mimi KAKA YAKO; " USIRUHUSU HIYO KITU" utakuja KUJUTA BAADAYE!.

Ukilala ni LIJAMAA tu Aisee 'UTAKUWA UMEFANYA UPUMBAVU KATIKA KANISA' 
Pia UTAKUWA UMEFANYA JAMBO LITAKALOIANGAMIZA NAFSI YAKO!. 

"KAMA HAJATAHIRIWA, HATUMPI MKE; akitaka mke huku SHARTI ni hili 'ATAHIRIWE KWANZA"

Mimi niishie hapo,
Natumai umenielewa, 
Mungu AKUBARIKI SANA KIJANA WA KANISA; MUNGU BADO ANATAKA AKUTUMIE, USIKUBALI HAYA MAMBO YAKAKUONDOA KWENYE MSTARI!. 

Ubarikiwe sana!. 

Na. Mwl. Nickson Mabena
(whatsapp #) 0712265856

admin