Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | KAMA ALIVYOSEMA ~ Sehemu ya 2

10
0

Ninakusalimu kupitia Jina zuri Jina la Yesu Kristo!

Karibu tuendelee na somo hili, huu ni mfululizo wa pili wa somo hili.

Kwenye sehemu ya kwanza ya somo niliweka utangulizi pamoja na kuelezea pointi moja kati ya tano nilizokupa.

Niliahidi kuendelea na pointi nyingine kati ya zile tano, lakini sitafanya hivyo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu; hivyo naomba nikuletee ujumbe kutokea kwenye MSTARI UFUATAO;-

Yoshua 6:26

"Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo."Yoshua 6 :26

Baada ya Mji wa Yeriko kuteketezwa na Wana wa Israeli, Yoshua aliwatuma watu wamtoe Rahabu pamoja na ndugu zake, Kisha Yoshua AKAMHIFADHI RAHABU na FAMILIA YAKE PAMOJA NA VITU VYAKE VYOTE!

Biblia inasema KWA SABABU ALIWAFICHA WAJUMBE ALIOWATUMA YOSHUA ILI KUUPELELEZA MJI WA YERIKO.

 Nataka nikuonyeshe vitu kutokea kwenye Mstari huo wa 26,

Yoshua ALIWAAPISHA KWA KIAPO, 'AKASEMA' Mtu akitokea akaujenga tena MJI ULE WA YERIKO alaaniwe;

Mambo mawili yatokee

  1. Atafiwa na MZALIWA WAKE WA KWANZA atakapouweka MSINGI wa Mji huo.
  2. Atafiwa na MTOTO wake mdogo wa kiume.

YOSHUA ALITAMKA TU KWA KINYWA CHAKE;

Najaribu kufikiri hapa, Kama WATU wa Kanisa la Leo wangekuwa wanamsikia Yoshua ANATAMKA MANENO HAYO wangemuelewaje?

Najaribu tu KUFIKIRI,

Mkristo wa Leo angemsikia Yoshua ANATAMKA hayo maneno WANGEMPA JINA GANI?

Najua utaniambia kwamba TUPO KWENYE AGANO JIPYA; HATUPASWI KUTAMKA LAANA YOYOTE, TUMEAMRIWA KUBARIKI NA SIO KULAANI..

Nikubaliane na wewe kwenye hiyo,

Nageuza kidogo tu maneno hayo,

Chukulia Yoshua ni Mchungaji wa Kanisa 'X', alafu ukamsikia ANAWATAMKIA MANENO WA USHINDI/MAFANIKIO WASHIRIKA WAKE WANAOONEKANA (KWA MACHO) ni CHOKA MBAYA, ungemuinaje huyo Pastor?

 

Mchungaji kama huyo, kuna maneno akiyatamka mbele ya WACHUNGAJI wenzake WATAMUONA AMECHANGANYIKIWA!

Tuangalie kwanza kilichotokea baadaye kwanza, alafu nitakwambia kitu kabla sijamaliza!

Biblia inasema;

 

"Katika siku zake, Hieli Mbetheli AKAJENGA YERIKO; akatia misingi yake KWA KUFILIWA NA ABIRAMU mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa KUFIWA NA MWANA WAKE MDOGO Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni" 1Wafalme 16:34,

 

Nina Hakika Hieli alikuwa hataki KUFIWA na watoto wake;

Alienda AKAUJENGA YERIKO TENA, kumbe kuna MTU ALISHAWAHI KUSEMA UKIJENGA YERIKO TU; KUNA VIFO VITATOEA..

Hieli alipoujenga YERIKO; aliondokewa na WATOTO wake 'KAMA YOSHUA ALIVYOSEMA';

Ukiulizia jamani watoto walikuwa na tatizo gani hata wakafa? Utaambiwa wamekufa "KAMA YOSHUA ALIVYOSEMA "

Pengine watu HATA YOSHUA MWENYEWE HAWAMJUI, lakini wanaambiwa tu "KAMA YOSHUA ALIVYOSEMA".

Kwa nini na wewe Mtumishi wa Mungu USITAMKE VITU KATIKA ROHO MTAKATIFU?

Haijalishi MAZINGIRA ya sasa YANAONYESHA hakuna dalili ya kutokea UTAKACHOKITAMKA kwa kinywa chako, WEWE TAMKA kwa HAKIKA MOYONI ipo siku YATATOKEA HATA WEWE USIPOKUWEPO!

Wakati ZEKARIA anatamka kuhusu PUNDA (rejea Sehemu ya kwanza); ILIPITA MIAKA MINGI SANA hadi ILIPOKUJA KUTOKEA!

Mazingira ya sasa yasibadilishe USEMI WAKO; Mazingira ya sasa yasitengeneze hatima yako;

TAMKA MANENO KWA UJASIRI, MANENO YANAISHI, MANENO HAYAFI; Kwa nini UOGOPE?

Sijui nikupe shuhuda ili unielewe vizuri!?Muwekee Shetani UZIO katika ulimwengu wa roho ILI ASIKUZOEE TENA, Yazuie MAGONJWA kwa KINYWA CHAKO hakika hayatakutesa tena,

Hiyo tabia usiyoipenda KWA NINI BADO UNAILEA LEA? unasubiri uwekewe mikono? Hahaha.. Unacho kinywa bhana IFUNGIE NJE HIYO TABIA,

Zuia vitu VIOVU VYOTE KWA WATOTO WAKO (YERIKO ISIJENGWE TENA KAMA WEWE ULIVYOSEMA);

kama umeridhika 'kupigwa vibao' kila siku na yule ADUI, endelea tu; lakini kama HUJARIDHIKA, MUWEKEE MPAKA KWA MDOMO WAKO!

ninajua "YERIKO HAUTAJENGWA TENA; KAMA WEWE ULIVYOSEMA"

Kwa nini kila siku wewe tu ndio UNAANGUKA?

unakipenda hicho KIFAFA? ZUIA KUANGUKA!

Nimalizie kwa kusema hivi,

"KUNA VITU VITAKUJA KUTOKEA KWAKO, MUDA MCHACHE UJAO; KAMA WEWE ULIVYOSEMA".

Mungu akubariki, Tukutane kwenge sehemu ijayo, Naamini utafuatilia tena,

 

Na: Mwl. Nickson Mabena

       (WhatsApp#) 0712265856

        Email: mabenanickson@gmail.com

       ©Kagera, Nchi ya Maziwa na Asali

admin