Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | KAMA ALIVYOSEMA ~ Sehemu ya 1

11
0

Haleluyah Mtu wa Mungu upendwaye sana! Jina langu naitwa Mwl. Nick

Ninayofuraha kubwa kupata neema ya Kukuletea UJUMBE WA NENO LA MUNGU;

Karibu tujifunze saa hii! "Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda."ZEK. 9:9

Zekaria ni mmojawapo wa MANABII waliotoa UNABII kuhusu Yesu Kristo,

Ukisoma kitabu cha Zekaria utakutana na NABII kadhaa zinazomuhusu Masihi wa Bwana Yesu Kristo au zinazohusu Nyakati za Yesu (Matukio yatakayofanyika/yaliyofanyika wakati wa Yesu).

Zifuatazo ni Baadhi ya NABII hizo, alizozitabiri Zekaria;-

  1. Yesu kuingia Yerusalemu akiwa amempanda mwanapunda (Zek 9:9)
  2. Yuda kumsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha (Zek 11:12-13)

           👉Yeremia alitabiri pia kwenye Yer 32:6-9.

  1. Yesu kuuawa kama Mchungaji (Zek. 13:7)

👉Andiko hili Yesu pia alilinukuu kwa kinywa chake; (Mathayo 26:31)

  1. Yesu kukanyaga tena kwenye Mlima wa Mizeituni (Zek. 14:4)
  2. Yesu kutawala kama Mfalme (Zek. 14:9)

 

Kutokana na Ujumbe nilionao kwako, nitazungumza kidogo kutokea kwenye NABII KAMA MBILI HIVI kati ya hizo tano nilizokutajia hapo Juu!

Pamoja na hayo, nakupa Shauri; tafuta muda mzuri uzifuatilie kwa karibu hizo NABII.

Ninakwambia hivyo kwa sababu, njia mojawapo ya KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU ni kwa kuzifuatilia NABII za aina mbili zinazomzungumzia Yesu,

 

  1. Zilizotabiriwa zikatimia.
  2. Zilizotabiriwa ambazo bado wakati wake kutimia.

(Sio somo langu la Leo)

Turejee kwenye SOMO!

 

Nikianza na ile ZEKARIA 9:9, utaona Nabii anatabiri kwa habari ya Yesu KUINGIA YERUSALEMU AKIWA AMEMPANDA PUNDA/MTOTO WA PUNDA,

Nabii aliishi miaka mingi kabla ya Yesu KUZALIWA,

Lakini aliona katika Roho kwamba kuna wakati utafika ambao MFALME ATAINGIA YERUSALEMU AKIWA AMEMPANDA PUNDA..

Wakati ulipofika, Yesu aliwaambia wanafunzi wake

"Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwanapunda, pamoja naye; wafungueni mniletee" MATHAYO 21:2

 

Tusogee tena kidogo

"Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake" MATHAYO 21: 6,7

Alichokisema Zekaria kikatimia kwa staili hiyo, ni sahihi?

Sasa, tafakari na mimi;

Ingetokea nikawauliza wale wanafunzi wa Yesu "KWA NINI HUYU PUNDA NA MWANAPUNDA WAMEFUNGWA HAPA?"

hivi wangenipa Jibu gani? Wewe Je! Utanipa Jibu gani?

(Kabla sijakusaidia hiyo ya kwanza)Tafakari nyingine, KWA NINI YESU AINGIE YERUSALEMU AKIWA AMEMPANDA PUNDA? (yawezekana unalo jibu hapa).

Kwa tafakari hizo MBILI utaanza kunielewa nitakachokufundisha kwenye somo hili;-

Mimi ninaona hivi "YESU ALIINGIA YERUSALEMU AKIWA AMEMPANDA PUNDA KAMA ZEKARIA ALIVYOSEMA"

kwa hiyo; yule Punda na Mwanapunda WALIFUNGWA pale kwenye kile Kijiji ili waje WAMBEBE YESU na kuingia naye Yerusalemu 'KAMA ZEKARIA ALIVYOSEMA'

Kwa hiyo; Endapo ZEKARIA asingesema kwamba MFALME (Yesu) ATAINGIA YERUSALEMU akiwa AMEMPANDA PUNDA inawezekana YESU ASINGEMPANDA YULE PUNDA;

Lakini pia, Kama Zekaria ASINGESEMA vile inawezekana YULE PUNDA NA MWANAPUNDA WASINGEFUNGWA KWENYE KILE KIJIJI!. Kama ni hivyo basi,

Kumbe YAWEZEKANA KABISA kuna MAMBO YAPO KWENYE MAISHA YAKO, KWA SABABU 'ZEKARIA' ALIYASEMA MIAKA KADHAA HUKO NYUMA,

Yawezekana pia UPO HIVYO ULIVYO ikiwa ni MATOKEO ya 'ZEKARIA' WAKO KUTAMKA HUKO NYUMA KABLA YAKO KUZALIWA!

 

(Afadhali Zekaria wako awe MTUMISHI WA BWANA, kuliko kama ni MTUMISHI WA SHETANI)

Nisikuaminishe sana kwa 'Zekaria' waliopita (PENGINE HUAMINI KATIKA HAYO)

Msukumo wangu kupitia UJUMBE huu wewe uwe 'ZEKARIA' wa Leo;

UTAMKE MAMBO KWA AJILI YA MAISHA YAKO, FAMILIA YAKO, NDOA YAKO, MASOMO YAKO, WATOTO WAKO, AFYA YAKO, MUME/MKE WAKO, HUDUMA YAKO n.k,

Utamke mambo katika Roho Mtakatifu ili siku zijazo yakitokea TUKUMBUKE na kusema "KAMA ALIVYOSEMA" Kupitia Kunywa Chako UNAWEZA YAKAZALIWA MAMBO MAZURI SANA,

UNAWEZA ukatamka na "Punda na Mwanapunda wakafungwa" kama ULIVYOSEMA!

Tamka Leo KATIKA ROHO ili vizazi vyako VIJE KUYAFAIDI HAYO UNAYOYATAMKA LEO;

Yerusalemu kulitaharuki kwa nderemo na vifijo na shangwe 'KAMA ZEKARIA ALIVYOSEMA'.

Wewe unatamka NINI LEO?

......Nitaendelea na somo hili,

Usiache kufuatilia,Kama kuna kitu umekilata mshirikishe na mwenzako,

 

Na: Mwl. Nickson Mabena

WhatsApp# 0712265856

admin