Skip to main content

MWL. NICKSON MABENA | FANYA MAANDALIZI KWA UJIO WA YESU/KUKUTANA NA YESU

18
0

Yesu Asifiwe MPENDWA wa Mungu,

Ninayo furaha kubwa kukukaribisha kwenye ujumbe huu muhimu kwa ajili ya Kanisa!

Hatuna namna tunaweza tukabadilisha ukweli kwamba YESU ANARUDI,

Uwe unapenda au hupendi lakini YESU ANARUDI, Uwe unaamini au huamini ukweli utabaki kuwa YESU ANARUDI,

Uwe UMEJIANDAA Kumpokea au hujajiandaa bado YESU ANARUDI, Kwa vyovyote vile YESU ANARUDI!.

Biblia inasema kwamba KILA JICHO LITAMWONA, Waliolala katika KRISTO YESU, WATAFUFULIWA KWANZA ndipo walio hai watafuatia kumlaki YESU.

 

Kwenye SOMO hili nitazungumza zaidi KUTOKEA kwenye mfano wa WANAWALI KUMI;

 

Unawakumbuka hao WANAWALI? Kama huwakumbuki usijali, nitakukumbusha kidogo kidogo na mwishowe UTANIELEWA VYEMA;

Habari za WANAWALI KUMI zipo katika kitabu cha Mathayo 25:1-13. Biblia inasema WANAWALI WATANO WALIKUWA WAPUMBAVU na WATANO WALIKUWA WENYE BUSARA;

 

Maandalizi ya kumlaki bwana arusi ndio yaliyowatofautisha WANAWALI HAWA!

 

Kwa nini?

 

Kwa sababu

"Wale waliokuwa WAPUMBAVU walizitwaa taa zao, wasitwae MAFUTA pamoja nao; bali wale WENYE BUSARA walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao" MATHAYO 25:3-4

 

Hawa jamaa wamebeba TAA lakini hazina MAFUTA; wenzao 'WAKAJIONGEZEA' Kamzigo kidogo; WAKABEBA TAA NA MAFUTA..

 

Walipoendelea sana KUSUBIRI wakaona kama vile bwana arusi AMEGHAIRI hivi kurudi; WOTE WAKALALA USINGIZI,

 

Lakini 'USIKU WA MANANE'

 

ndipo bwana arusi akaingia; TOFAUTI IKAONEKANA KATI YA WALIOJIANDAA KUMLAKI na ambayo HAWAKUJIANDAA VYEMA (WAPUMBAVU).

WEWE UMEFANYA MAANDALIZI YA KUKUTANA NA YESU KWENYE KITI CHA HUKUMU?

UMEJIANDAA KUMLAKI BWANA YESU?

Wewe ni miongoni mwa WANAWALI WENYE BUSARA au WAPUMBAVU? (Itajulikana zaidi kwamba nani ni nani pale bwana arusi atakapotia maguu).

 

Kabla bwana arusi hajafika, wote walionekana kama vile WANA SIFA ZA KUMLAKI; lakini alipofika NDIO IKAJULIKANA NANI ANAZO SIFA ZA KUMLAKI BWANA YESU!

 

Shauku yangu ni hii; PAMOJA NA KUTUMIKA, PAMOJA NA KUTAFUTA MAISHA, PAMOJA NA KUWEKA MALENGO, PAMOJA NA KUWA NA HUDUMA MBALIMBALI pamoja na yote hayo BADO TUNATAKIWA KUWA TAYARI KUMPOKEA YESU au KUKUTANA NA YESU!

 

Ni MBAYA sana, KUTUMIKA kote huko ALAFU UIKOSE MBINGU;

 

Mpendwa USIJISAHAU,

YESU YUPO MLANGONI,

 

Anarudi "USIKU WA MANENE"

 

Wakati ambao WATU WAPO BIZE NA UTUMISHI huku WAMEACHA UTAKATIFU,

 

Wakati ambao WATU WAMEJISAHAU, WAMELALA WAKIDHANI BWANA YESU 'AMEGHAIRI' KUJA;

 

Tafuta kwa bidii KUWA NA AMANI NA WATU WOTE, NA HUO UTAKATIFU.. Ndio NA HUO UTAKATIFU!

 

UTAKATIFU hautafutwi baada ya KUFA (BAADA YA KIFO, HUKUMU);

 

Utakatifu UNATAFUTWA SASA HIVI, Nyakati hizo unazozifikiria KWAMBA utatafuta utakatifu UTAKUWA UMECHELEWA NDUGU YANGU!

 

"Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa" MATHAYO 25:10

 

Mlango wa NEEMA upo wazi sasa hivi; Usiringe na DINI yako wakati HUNA YESU, ni sawa na kubeba taa bila MAFUTA,

 

Usiringe na HUDUMA yako bila YESU, usiringe na NABII WAKO, MTUME WAKO MCHUNGAJI WAKO, PAROKO WAKO bila kuwa na YESU NI BURE TU!.

 

FANYA MAANDALIZI YAKO BINAFSI, UWE TAYARI WAKATI WOTE; HATUJUI SIKU WALA SAA ATAKAYORUDI BWANA YESU, WALA HATUJUI SIKU WALA SAA UTAKAYOONDOKA DUNIANI

 

Chagua KUOKOKA!!.

 

Ubarikiwe,

 

Na: Mwl. Nickson Mabena

     (WhatsApp#) 0712265856

 

admin