Skip to main content

MWL. ISAYA KAKUSA | JIFUNZE KUOMBA ROHO YA KUTOZIMIA WALA KUCHOKA TOKA KWA MUNGU IKUSAIDIE KUKAMILISHA MAKUSUDI YAKE MAISHANI MWAKO

9
0

Isaya:40.28

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Isaya:40.29

Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

Isaya:40.30

Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

Isaya:40.31

bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

 

Bwana Yesu asifiwe sana sana.

Kuto kuzimia wala kuchoka ni tabia ya  kiungu , iko ndani ya Moyo na Roho wa Mungu.

Unapoamua kumgeukia na kumfuata Mungu hii tabia uwa inawekwa ndani ya watoto wa Mungu.

Si vyema kwa mtoto wa Mungu kuzimia na kuchoka njiani.Ukiona unakatabia ka kuzimia na kuchoka.

 

Rudi magotini mwa Mungu kwa upya na uanze kuomba rehema zake juu yako.

 

Rehema za Mungu ni kule kukuonea huruma na kukupa msaada juu ya tatizo lako la kuchoka na kuzimia zimia njiani.

 

Kukata tamaa sio tabia ya Kiungu , unapokata tamaa njiani na kuzimia na kuchoka hapo tambua kuwa kuna upungufu fulani wa nguvu za Kiungu ndani yako umekupata.

 

Mithali 24:10 inatueleza ivi ;

 

Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.

 

Ukiona unazimia na kuchoka juu ya jambo fulani ulilokuwa unalitazamia kwa Mungu na unajisikia kukata tamaa ya kuliombea hapo ujue wazi kwamba nguvu zako ni chache zile za Kiungu ambazo tunazipata kwa kufanywa wana wa Mungu kwa Roho Mtakatifu

 

Sasa usianze kutoa sababu za kibinadamu na kujitetea na kujihesabia haki ,we rudi kwa Mungu mapema na kuomba toba bila kusita kwa sababu huko kuzimia na kuchoka sio tabia ya Mungu ,Mungu hazimii wala achoki sasa umepata wapi uo uchovu wa maombi na wa kiimani?

 

Lazima kuna mlango umewachwa wazi na adui amepanda mbegu ya udhaifu uko ndani ya moyo wako , rudi kwa Mungu haraka

 

Neno linasema kwenye Isaya 40:29 kuwa Mungu huwapa nguvu wazimiao , humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo

 

Usifanye haraka kuondoka mbele za Mungu wako unapokuwa unatarajia akujibu maombi yako ,kaa mbele za Mungu kwa imani ,we amini tu hata kama mambo ni mabaya na magumu sana amini tu.

 

Neno linasema kuwa sifa mojawapo ya kutiwa nguvu mpya na Mungu ni ya kuendelea kukaa mbele zake na kumngojea daima

 

Ukimngojea Bwana Mungu utapata nguvu mpya , utapandishwa viwango vingine vipya vya kiroho kama tai arukavyo kwa mbawa zake ,mbawa ni uwezo au nguvu utakazozipokea toka kwa Mungu na kuwa juu baada ya kumngojea

 

Mungu ataondoa kama ukimngojea ule uchovu wa kiroho uliokuwa ukiusikia ,utakwenda kwa miguu wala hautachoka na miguu ni kiwango au uwezo wako binafsi wa kutembea ndani ya kusudi ,sasa ule uwezo wako utaongezewa nguvu zaidi na utashangaa unakwenda mbali na lile kusudi bila kuliacha

 

Marufuku kukata tamaa kwa mwana wa Mungu.

 

Jipime kwa kiwango hiki cha neno ,je bado we ni mwana wa Mungu au la .

 

Jifunze kutafakari na uchukue hatua.

 

Na ISAYA KAKUSA 0718975690

WHATSAPP AU 0756443660

 

 

admin