Skip to main content

MR & MRS MWAKATWILA | JIFUNZE NAMNA YA KUULINDA MOYO WAKO (AU NAFSI) NA KUUTOA KWENYE MAANGAMIZO SEHEMU YA 23 (MWISHO)

20
0

Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana sana!!!

LEO TUNAPOMALIZA KUJIFUNZA SOMO HILI. Nataka kumshukuru Mungu aliye tupatia neema hii ya kujfunza somo hili. Kwangu nimeona nikijengwa mno moyoni mwangu. Naamini na kwako. Ebu mshukuru Mungu kwa kukufundisha tu. Mpe heshima Roho Mtakatifu alienipa nafasi hii ya kukuletea masomo haya.Chukua hatua ya kuyaweka kwenye matendo haya uliyojifunza.

Nimalize kwa kusema ombea somo lijalo. NA NIOMBEE MIMI NA FAMILIA YANGU ILI TUMTUMIKIE MUNGU VEMA.

Nakukaribisha darasani karibu ili tuendelee kujifunza . Katika kipindi kilichopita nilikuonyesha jambo lingine muhimu ambalo unatakiwa ulifahamu ili upate kuilinda na kuitoa nafsi yako au moyo wako katika maangamizo. Nilikuonyesha eneo la damu ya Bwana Yesu Kristo.

Leo nataka niendelee mbele kidogo hapo. Biblia inapotupa sisi agizo la kulinda moyo fahamu moja ya  ngao au zuio la hatari au kinga ya mambo mabaya Kibiblia ni damu. Ngoja nikupe mfano, Mungu alipokua anataka kuwakinga wana wa Israeli na jambo baya lililokua linakwenda kuondoa uzima na uhai wa watu waliokua kule Misri aliwapa agizo la kutumia damu ili kumzuia yule mharibu.

Maandiko yanasema hivi.  " Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka.Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi."(Kutoka 12:21-23).

 

Ukiipitia hiyo mistari utaona wazi kuwa damu ya kondoo huyo ilitumika kumzuia muangamizaji ambaye hapo anaitwa mwenye kuharibu asiingie kuwapiga hao ndugu. Kuna kitu cha kujifunza hapo. Mharibu huyo alikua analenga kuzipiga nafsi au mioyo ya watu ili kuiachanisha na mwili.

 

Unaposikia mtu furani kafa fahamu kunakua kumetokea utenganifu kwake kati ya nafsi na mwili wa huyo mtu. Unapoiondoa roho ndani ya mwili fahamu nafsi(PUMZI HAI) itaondoka na hiyo roho. Sasa kilichozilinda zile nafsi za wana wa Israeli ni damu maalumu ya kondoo aitwaye pasaka. Kitu kingine cha kujifunza hapo ni hiki. Mharibu huyo alitumwa na Mungu. Kama mharibu atumwaye na Mungu anaweza kuzuiwa kwa damu fikiria mharibu atokaye kwa shetani si ndiyo atakimbia kabisaaaa.?

 

Ili sisi leo hii tupate kuzilinda nafsi zetu au hiyo mioyo yetu na mharibu atakaye kuharibu hisia zetu, utashi wetu, mawazo yetu fikra zetu kutafakali kweli akili zetu.  Mungu alitupa kinga hii iitwayo damu ya Yesu Kristo. Maandiko yanatufundisha wazi kuwa Bwana Yesu Kristo ndiye pasaka wetu sasa.

 

Angalia mistari hii isemavyo."Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;"(1Wakorintho 5:7).

 

Ukiipitia hiyo mistari utaona Bwana Yesu ndiye pasaka wetu leo. Pasaka yule alitoa damu, na pasaka huyu nayeye ametoa damu. Kama damu ya pasaka yule ilimzuia mharibu fahamu hata damu ya pasaka wetu Yesu Kristo inauwezo zaidi ya kumzuia mharibu wa nafsi zetu yaani shetani. Biblia inasema damu ya Yesu inaweza kushughulikia mpaka dhamiri ya mtu au mfumo mzima wa akili za mtu.

 

Angalia mistari hii "basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?"(Waebrania 9:14).

 

Damu hii inaweza kushughulikia dhamiri ya mtu kabisaa. Neno dhamiri ukiliangalia kwa undani unaona ni nia au fkra au mfumo mzima wa ufahamu wa mtu tunaita akili. Huko ndani kuna mawazo,fikra, kutafakari nk. Sasa Mungu alipoona mfumo wa akili za mtu hauko sawa akaamua kututafutia dawa au nyezo ya kuitengeneza(takasa) akatupa hiyo damu ya Bwana Yesu Kristo. Biblia inaposema mgeuzwe nia zenu anamaana nia zetu au dhamiri zetu au fkra zetu zimeharibiwa. Swali tunageuzwa na kitu gani?

 

Ukiiangalia utaona damu ya Yesu inauwezo wa kushughulikia dhamiri  au nia zetu zilizogeuzwa na shetani.  Damu ya Yesu Kristo inaweza kujenga kabisaa moyo wa mtu ulioharibika. Kumbuka damu ina uhai, inasema, inasikia,inaweza fanya kitu.

 

Ngoja nikufundishe kitu  hiki. Ninaposema damu ya Yesu njoo moyoni mwangu fahamu  itatega sikio lake isikilize huyu mtu ananiitaji moyoni mwake ili nikafanye nini?

Ukiiambia njoo moyoni na unitakase itakuja na kukutakasa, ukiitaka ije moyoni na kujenga palipobomoka itakuja kujenga.

 

 Ngoja nikupe mifano hii ili imani yako iongezeke katika jambo hili. Biblia inasema hivi. "( na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi."Waebrania10:22).

Mioyo yetu ili iondokane na ubaya wa aina yoyote inahitaji kitu cha kunyunyuziwa. Mimi naita dawa ya kunyunyuzia mahali palipo dhaifu. Najua unafahamu aina mbalimbali za dawa. Ukiwa na kidonda kuna dawa za kupaka kunywa kunyunyuzia nk. Sasa angalia kitu hiki. Kama moyoni mwako unakidonda cha uchungu hivi, hisia zako zimejeruhiwa na kuna kidonda kitoacho usaa kabisaa.

 

Utatakiwa kwanza usafishe hicho kidonda, hapo kuna maji yatokayo ubavuni mwa Bwana Yesu Kristo. Nyunyuzia hayo maji. Maandiko yanasema hivi."Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama."(Ezekieli 36:25-26).

 

Maji hayo yapo kabisaa leo hii. Aliyatoa Bwana msalabani. Yapo kama vile leo hii damu ipo. Yanatafuta watumiaji tu. Sasa sikia safisha moyo uliojeruhiwa kwa maji hayo. Harafu nyunyuzia hicho kidonda kwa damu ya Bwana Yesu Kristo.  Utaona taratibu dhamiri zao mbaya  au hisia zako zilizoumizwa au mawazo yako na  fikra zako  ziliogonjwa zinaanza kuponyeka.

 

Watu wengi wanahisia zilizojaa vidonda vya wivu, husuda, chuki, kutokupendwa, kujeruhiwa na mume, au boss kazini, yaani wanatembea na vidonda ambavyo viko nafsini na visipotibika haraka vinaleta madhara yake mpaka kwenye mwili. Ndiyo unadikia bp vidonda vya tumbo, msongo wa mawazo nk.

 

Kama unataka kulinda moyo au kuutibu unaweza tumia damu ya Bwana Yesu Kristo. Mwingine anasema nilijaribu sijaona matokeo? Nakuhakikishia hukumaliza dawa!!!! Watu wengi wanapotaka kutibu mioyo yao iliyojeruhiwa WANATATIZO LA KUTOKUMALIZA MATIBABU YAO!!!!

 

Utaona mtu kaanza asubuhi kuomba maombi ya mfumo huu. Jioni haombi, kesho haombi, atakuja kuomba jumapili.Siku zingine zote msikilize, anamaombi ya kisasi kwa watu au ndiyo  anaomba Mungu ampe fedha weeee!! Mungu anakupaje fedha wakati ni mgonjwa wa tamaa kwa wanawake? Si sitakuvuruga hizo fedha mpendwa? Tibu kwanza ugonjwa ndipo uombe fedha.

Mwingine ndiyo anaomba upako mkubwa weee wa huduma yake. Sikia. Mungu hawezi kukupa upako huo kwasababu wewe ni mgonjwa wa kiburi, majivuno, mashindano nk. Ukikazana kupokea tiba ya kunyunyuziwa damu ya Yesu moyoni mwako na ukapona ugonjwa wa kiburi, nakuhakikishia wala hutaomba kwa urefu kuhusu upako. Utashushiwa hata bila kuomba nakuambia.

 

Kinachotuzuilia baraka zetu nyingi ni matatizo tuliyonayo moyoni. HILI NDILO TATIZO KUBWA MNO LILILOWAKABILI WATOTO WA MUNGU WENGI. Fikiria kidogo wewe ni mgonjwa wa uizi, Mungu anakupelekaje leo hii ukafanye kazi benki? Mungu anajua kabisaa huyu mwanangu ni ni mgonjwa kwenye eneo la ukatili, anakupaje uongozi? Mpaka utibiwe kwanza.

Ninachotafuta hapa ni hiki. Anza kuitafuta damu ya Bwana Yesu Kristo kama sehemu ya tiba ya moyo wako uliojeruhiwa. Omba utakaso ikutakase, iambie ikujengee mfumo mzuri wa moyo wako  iambie ikulinde dhidi ya mharibu ashambuliaye mioyo nk.

 

Unajua ninapokuambia ikujengee huko moyoni unaweza kufikiri hivi damu inaweza jenga kitu  kweli? Angalia mistari hii."Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga."(Waefeso 2:13-14).

 

Ukiipitia hiyo mistari utaona damu ya Yesu ilikibomoa kiambaza kilichokua kinatutenga sisi wamataifa na Wayahudi. Kilichotufanya tuwe karibu ni damu ya Yesu. Sikia kama damu hii inaweza bomoa kiambaza unafikiri haiwezi jenga kiambaza?

 

 Katika ulimwengu wa roho damu inatumika kujenga mambo kabisaaaa!!!! Na damu hii inaweza bomoa viambaza vya aina yoyote. Tumezoea kusema ngome. Kama akili zako zimezunghushiwa ngome na fikra zako zimetekwa huwazi sawasawa unawaza madeni tuuuu!! Misiba tuuuu, wanawake tuuuu!!! Au unawaza waliokujeruhi tuuu!!! Sikia bomoa hiyo ngome iliyokuzunguka katika mawazo yako kwa kutumia damu ya Yesu Kristo.

 

Inawezekana kuna mtu moyoni mwako humpendi kabisaa na umejitambua wazi kuwa wewe hapo ni mgonjwa. Anza kufanya maombi maalumu tumia damu ya Yesu kuiondoa hiyo tabia ya chuki moyoni mwako. Mimi nakuhakikishia ukiamini utauona mkono wa Mungu akiitumia damu yake kukutengenezea upendo kwa huyo unaye mchukia.

 

Maandiko yanasema wazi damu hii ya Bwana Yesu Kristo inaweza kukutoa katika kifungo au tabia furani iliyokukandamiza. Maandiko yanasema hivi."Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji. Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba nitakurudishia maradufu."(Zekaria 9:11-12).

 

Damu inaweza kumtoa mtu kwenye kifungo kilichomfunga. Angalia umetumbukia kwenye shimo la aina gani? Ni ulevi? Ni uzinzi? Ni kifungo gani kimekufunga huko moyoni? Ni hasira? Ni nini ni kutokuamini? Ni kutokuelewa? Ni kifungo cha kukata tamaa moyoni na kutokujiamini? Ni shimo gani umetumbukia ni dhambi? Usikawie iite damu ya Bwana Yesu Kristo kwa imani. Itakutoa kifungoni

 

Si kukutoa tu. inaweza kukuludishia vile ulivyopoteza. Mfano. Ulipoteza amani na mtu au Mungu, ulipoteza heshima, ulipoteza uwezo wako wa kufikiri yaani mfumo wa akili zako hauko sawa. Ngoja nikupe mfano, unapo ingia katika mahusiano na mtu asiye mwaminifu kitakachotokea ni umivu moyoni. Na akikujeruhi mpenzi uwezo wako wakiakili unapotea kabisaaa.. Sasa ili uludishiwe ulichopoteza yaani akili unatakiwa uanze kuomba maombi maalumu kwa kuitumia hii damu ya mjumbe wa agano jipya yaani Bwana Yesu Kristo.

Inawezekana ulifiwa na mpaka sasa moyoni haujakaa sawa kabisaa anza kuitumia damu hii ikusafishe na iruhusu ikutengenezee kwa upya mahali palipo haribika. Damu ya Yesu inauwezo mkubwa mno mno. Kumbuka inauhai kabisaa, inanena mema. Kinachonenwa huumbwa katika ulimwengu wa roho. Unapomuamini Bwana Yesu Kristo na ukaamini kuwa alitoa damu yake ya aina hii anza kuitumia damu hii kwa faida.

 Niliwahi kusikia ushuhuda wa mtu aliyeumwa na nyoka mwenye sumu kali sana. Unajua alipogundua kaumwa tu. Aliitia damu hii ya Bwana Yesu Kristo na aliweka mkono mahali alipoumwa unajua hakufa kama watu wengine waliokua wakifa baada ya kuumwa na nyoka wa aina hiyo. Ebu angalia na wewe umeumwa na nyoka wa aina gani  na amekuachia sumu ya ainagani huko moyoni mwako? . Kumbuka shetani ni nyoka na jamii yake yote ni nyoka na nge nk.

Sasa anza kuitumia damu hii kama tiba na nyezo ya kuukarabati moyo wako.

Naamini umenielewa

Mungu akubariki

Na: Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila

www.mwakatwila.org          

admin