Skip to main content

MR & MRS MWAKATWILA | JIFUNZE NAMNA YA KUULINDA MOYO WAKO (AU NAFSI) NA KUUTOA KWENYE MAANGAMIZO SEHEMU YA 21

24
0

Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana. Ninakukaribisha tena darasani. Kumbuka kuiombea semina tunayoendelea nayo pale Bethel na leo ni siku  yetu ya sita ndani ya siku nane. Ni Semina nzuri kwakweli. Tunamuona Mungu akituvusha sehemu moja na kutupeleka sehemu ya pili kiimani.

 

Ebu tuanze kujifunza. Katika kipindi kilichopita  tulijifunza namna ya kutumia kinywa chako iliupate kuijenga nafsi yako au ya mtu mwingine.  Leo nataka tusogee mbele tena. Tuangalie jambo lingine ambalo unaweza kulitumia katika kuijenga nafsi yako iliyobomolewa nayo ni hii.

JIFUNZE KUOMBA KWA ROHO KWA MUDA MREFU.

Nisikilize kwa makini. Unaposoma maandiko matakatifu unagundua wazi kuwa Mungu. Alipokua analeta au anatupa kipawa cha kunena kwa lugha mpya alikusudia mambo furani muhimu. Sikia neno la Mungu linatufundisha kuwa kipawa au karama ya kunena kwa lugha imebeba ndani yake mambo mengi sana. Ndani ya kipawa hicho kumebebwa ishara mojawapo ya kuwa unamwamini Mungu.

Maandiko yanasema hivi "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;"(Marko 16:17). Kunena kwa lugha ni miongoni mwa ishara zimtambulishazo mtu kuwa anamuamini Bwana Yesu Kristo. Sikia nasema ni moja wapo ya ishara au dalili zinazotumika kumtambulisha mtu kuwa anamuamini Yesu.

Zipo ishara nyingi tu zinazotumika kumtambulisha mtu kuwa anamuamini Bwana Yesu Kristo. Nikitaka kukufahamisha zote naona hapo sitatoka mapema. Yaani ni somo lingine kabisaa. Ninachotaka kukujulisha  hapo ni ishara hii ya kunena kwa lugha. Lakini lazima ujue zipo nyingi kimaandiko.  Ndani ya kipawa hiki pia kuna roho yako  kuzungumza na Mungu.

Maandiko yanasema hivi."Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake"(1Wakorintho 14:2). Ukiangalia hapo utaona kazi mojawapo ya kipawa hiki cha kunena kwa lugha ni hiyo ya  roho ya mtu kuzungumza na Mungu.

Pia ndani ya kipawa hiki ndiko kunakozaliwa neno la unabii. Sikia. Ukinena kwa lugha na ukapewa kufasiriwa kile ulichokua unaomba, ndipo upewapo neno kutoka katika ulimwengu wa roho ndilo liitwalo unabii. Unabii si neno litokanalo na akili ya mtu. Ni neno litokalo kwenye ulimwengu wa roho. Ukitoa neno lako mwenyewe hata kama umechukua mstari wa Biblia hilo si neno la kinabii. Labda iwe umesikia kutoka katika ulimwengu wa roho kuwa SOMA MSTARI FURANI NA MPE NENO HILO FURANI HAPO NDIPO TUNAITA UNABII.

Pia karama hii ya kunena kwa  lugha ndani yake imebeba nguvu ya kuijenga nafsi ya mtu iliyobomolewa au kuharibika. Maandiko matakatifu yanasema wazi kuwa mtu anenaye kwa lugha anafanya pia kazi njema ya kuijenga nafsi yake. Angalia mistari hii jinsi isemavyo. "Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake;"(1Wakorintho 14:4A).

Ukiipitia mistari hiyo utaona wazi kuwa  nafsi au moyo ulioharibika unaweza kujengwa kwa kutumia kipawa hiki cha kunena kwa lugha. Watu wengi leo hii wamepewa kipawa hicho lakini bahati mbaya hawajui kukitumia katika mambo mengi sana. Ngoja nikupe mfano mzuri. Ukiona hisia zako zimeharibika au utashi wako hauwezi kufanya maamuzi sahihi unajikuta umefanya usilolitaka fahamu unahitaji kujengwa ndani yako. Na moja ya nyenzo ya kukujengea nafsi ni kunena kwa lugha.

Unachotakiwa ukifanye ni hiki. Nena kwa malengo. Namaana hii. Tafuta muda wa kutosha tu, jitenge au kaa mahali pa utulivu anza kuomba kwa akili yaani omba kwa lugha ambayo akili zako  zinaielewa. Omba ukipeleka hitaji la kujengwa nafsini.

Omba kwa muda mchache pia jiruhusu sasa unene kwa lugha kea muda mrefu, HUKU NDANI YAKO UKIWA NA WAZO LA KUJENGWA MOYONI. Mungu atayaangalia mawazo yako yanataka nini. Maandiko yanasema hivi." Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;"(Waefeso 3:30)

Mungu anaweza kujua yale unayoyahitaji kwa kuangalia mawazo yako. Sasa unaponena huku ukiwa unawazo kusudiwa moyoni la kujengwa moyoni mwako fahamu Mungu atatumia nafasi hiyo kuijenga hiyo nafsi yako. Mfano unaona moyoni mwako kuna huzuni kubwa mno na hujui imeanzia wapi au unajua chakufanya wewe neno kwa muda mrefu utashangaa moyo wako uliobeba huzuni unajazwa  furaha.

Chukua muda kuyasukuma maombi ya mfumo huo. Angalia Bwana Yesu alipokua anahuzuni rohoni mwake alitafuta maombi. " Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.  Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe."(Mathayo 26:37-39)

Aliwaambia waombaji waombe maombi ya mfumo huo  kwa lisaa limoja hivi. Hata wewe ukiona moyoni mwako hakuko vizuri yaani umejeruhiwa iwe na dhambi au uovu furani jifunze kuomba maombi ya kujengwa nafsini mwako kwa mtindo huo wa kunena kwa lugha.

Sikia jifunze kufanya maombi ya kufunga ili ujengwe nafsini mwako. Angalia mfano huu."  Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote

watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?  Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?"(Isaya 58:3-6).

Ukiipitia hiyo mistari utaona moja ya kazi ya maombi ya kufunga ni kufungua vifungo vya uovu. Fikiria neno kifungo maana yake ni SHIKAMANO KATI YA MWILI NA NA NAFSI. Mwili ndiyo uliobeba tabia za uovu  Na kama moyo wako umeshikwa na mwili Mfalme Daudi anasema nafsi yake imeambatana na mavumbi angalia asemavyo. "25 Nafsi yangu imeambatana na mavumbi, Unihuishe sawasawa na neno lako."(Zaburi 119:25).

Nafsi ikishikwa na mavumbi au mwili fahamu itayatenda ya mwili tu. matendo yote ya mwili ni maovu tu. ukiona Mungu anasema watu hawa wanawaza mawazo maovu tu, fahamu wanayawaza mambo ya mwili. Ambayo ni uizi, uongo, wivu, uchawi, ukali, hasira, uzinzi, uasherati   Uchafu nk.

Sasa ili ufungue kifungo kilichoifunga hiyo nafsi yako na mwili( patano) unatakiwa uombe. Sasa ukiomba kwa kunena nakwambia utafunguliwa na nafsi yako itajengwa. Naamini umenielewa.

Barikiwa sana.

Na: Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila                       

admin