Skip to main content

MR & MRS MWAKATWILA | JIFUNZE NAMNA YA KUULINDA MOYO WAKO (AU NAFSI) NA KUUTOA KWENYE MAANGAMIZO SEHEMU YA 19

32
0

Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana.. Ni imani yangu kuwa unaendelea vizuri. Napenda kukutia moyo ndugu uliyeamua kuyafanyia kazi yale unayofundishwa humu darasani Kuwa kuna mabadiliko makubwa utayaona muda si mrefu. Fahamu nafsi yako inatengenezwa jipe moyo.

Ebu tuendelee mbele kidogo. Kumbuka katika kipindi kilichopita  tuliendelea kujifunza namna ya kuuponya moyo au nafsi iliyoshambuliwa na adui shetani. Ni likuonyesha eneo la Neno la Mungu

 

Leo hii nataka nikuonyeshe kitu kingine unachoweza kukitumia ili kuiponya nafsi yako au moyo wako. 

         

JIFUNZE  KUIPONYA NAFSI YAKO AU YA WENGINE KWA KUTUMIA KINYWA CHAKO

 

Unaposoma maandiko matakatifu yaani Biblia humo ndani utaona mambo ya ajabu sana. Moja ya jambo la ajabu ni hili la  Mungu kumpatia mtu mdomo kwa makusudio mengi sana. Moja ya kusudio la kinywa ni kuumba vitu katika ulimwengu wa roho na katika ulimwengu huu unaoonekana.

Biblia inatufundisha kuwa mdomo au kinywa sehemu nyingine unaitwa ulimi unaweza kuumba kitu au kukitia uzima kitu au kukifisha kitu.  Mauti na uzima wa mtu umefungwa katika uwezo wa ulimi. Angalia mistari hii uone. "Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake."(Mithari 18:20-21)

 

Ukiisoma hiyo mistari utagundua kitu cha ajabu sana. Uzima wa mtu au kitu umefungwa ndani ya kinywa cha mtu. Hata mauti au angamizo la mtu pia limefungwa ndani ya kinywa cha mtu. Wasomao maandiko wanafahamu kwanini watu wanatakiwa wakiri mbele za watu kuwa wameokoka. Maandiko yanasema hivi.

 

"Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."(Warumi 10:8-10).

 

Ukiipitia hiyo mistari utaona nguvu au uwezo wa mdomo au ulimi katika kuumba kitu wokovu au uzima wa milele kwa mtu. Anasema unapokiri au kusema kuwa  Yesu ni Bwana wako na ukaamini kuwa yuko hai utaokoka. Na anasema ili uupate wokovu lazima uamini na kukiri kwa kinywa chako.

 

Fikiria kdogo. Kama kukiri kwako au kusema kwako leo kunaweza kukupatia wokovu kwa maana nyingine kukiri kwako au kusema kwako kunaweza kukupatia angamizo. Ninachotaka ukione leo hii ni namna ya kuupatia moyo wako wokovu au uponyaji kwa kutumia hichohicho kinywa chako.

Moyo au nafsi inaweza kuponywa kwa kutumia mdomo. Biblia inasema hivi."Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu."(Mithari 21:23). Ili leo hii wewe uulinde moyo wako au nafsi yako lazima uwe makini sana katika eneo la kusema kwako. Nafsi yako inaweza kuingia taabuni au uangamizoni kwa kutumia mdomo wako tu.

 

Kama kinywa kinaweza itia nafsi taabuni basi kinywa hichohicho kinaweza itia nafsi rahani. Angalia tunaona kuwa kinywa kina uwezo wa kumpatia mtu uzima au mauti. Angalia  Mungu anapotuambia tulinde sana mioyo yetu moja ya silaha tunayoweza kuitumia kuilinda hiyo mioyo ni kinywa au KUSEMA KWETU. Angalia tunaambiwa hivi. "Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu."(Mithari 21:23).

 

Ili tuilinde mioyo yetu na kuiponya lazima tuwe makini wapendwa kwenye eneo la kusema kwetu. Kile ukisemacho fahamu hakiendi bure kinaumba vitu. Watu wengi wanapoingia kwenye magumu furani hawajui kuwa huenda magumu hayo yameumbwa kwa kupitia kinywa tu. Kama si wao walisema basi kuna watu walisema.  Biblia inasema wazi kuwa ulimi unaweza kuumba mambo Kabisaaa.

 

Mungu ili aumbe jambo anatumia kile kilichosemwa na mtu. Angalia mistari hii uone.  "Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya."(Isaya 57:18-19).

 

Mungu anatupa akili hapo kuwa yeye anayaumba yale tuyasemayo kwa kutumia hii hii midomo yetu. Ukiiangalia hiyo mistari utagundua kuwa  ili Mungu aponye anaangalia kilichosemwa na watu. Anasema ntamponya, nitamludishia faraja zake MIMI NAYAUMBA MATUNDA YA MIDOMO. Ninavyoona hapo. Huyo mtu alipata jeraha au ugonjwa moyoni na mwilini. Hakua na faraja, alijaa huzuni na uchungu huyo mtu, na ninaona dhambi ndiyo ilikua chanzo cha kupigwa kwa moyo huo.

 

Mtu  huyo alihitaji uponyaji. Mungu alimponya KWA KUTUMIA KILE KILICHOKUA KIKISEMWA AU KUTAMKWA. Si kasema mwenyewe jamani kuwa ntamponya, mimi nayaumba matunda ya midomo!!!! Kuna kitu kilitamkwa na huyo mtu na watu wengine maandiko yanasema walimlilia huyo mtu. Hata wewe leo hii Mungu anaweza kukuponya huko moyoni mwako ulikojeruhiwa na kupoteza uzima au faraja kwa kupitia kile kisemwacho na wewe  mwenyewe.

 

Mtu aliyepoteza faraja  maana yake hata akili hisia na utashi wake hauwezi kuwa mzuri. Mawazo yake yanakua ngomeni kabisaaa.  Mtu yoyote yule atendaye dhambi hawezi kuwa na amani au faraja.  Maandiko yanasema hivi."Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.  Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka.  Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu."(Isaya 57:19-21).

 

Mtu mwenye sifa hizi hawezi kuwaza vema kabisaa si kajeruhiwa na mabaya ayatendayo moyoni mwake? Kumbuka tuliko toka. Dhambi inatumiwa na shetani kuiondolea uzima nafsi ya mtu. Saa tunajifunza hapa tunaiponyaje hiyo nafsi iliyobomolewa na dhambi, uchungu, nk. Ili uiponye tunaona kinywa kina husika sana.

 

Ngoja nikufundishe kitu. Kama umetenda dhambi  na unaona kabisaa moyoni umepigwa yaani umepoteza uzima. Unatakiwa utumie kinywa chako KUUNGAMA DHAMBI YAKO.  Umeona kinywa kinavyoanza kuumba uponyaji hapo?  Kuna kitu kinaitwa ungamo. Ungamo linafanywa kwa kupitia kinywa.

 

Ni kukisema kile ulichofanya. Si moyoni tu hata kwa kutumia kinywani. Unapokiri kosa nakwambia ukweli ndiyo dawa ya kwanza ya uponyaji wa  moyo wako. Mungu anatufundisha watoto wake anasema hivi." Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."(Yakobo 5:16).

 

Maandiko yanatufundisha hapo mambo mawili makuu yazaayo uponyaji. Anasema ungamaneni nyinyi kwa nyinyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Ohooo!!ili niponywe nafsi au moyo wangu uliyopigwa na shetani kwa kutumia siraha iitwayo dhambi ninatakiwa kwanza niungame dhambi yangu hiyo niliyoitenda na kumpa shetani nafsi ya kuipiga nafsi yangu.

 

Ngoja nikupe mfano. Wewe leo hii unajua kabisaa Mungu ametuambia tuhakikishe hatu ukalishi uchungu mpaka jua kuchwa. Sasa kuna mtu kakuumiza, umepata hadira na uchungu huko moyoni, ukaukalisha siku ya kwanza, mwezi, mwaka sasa miaka. Na uchungu huo ukazaa ugonjwa moyoni wa akili zako kushambuliwa yaani mfumo wa mawazo yako umeharibiwa huwezi tena kuwaza vema fikra zako unaona kabisaaa zimeharibiwa unapoteza kumbukumbu na unaona kabisaa bp hii hapa vidonda vya tumbo hivi hapa.

 

Yaani wewe ni mgonjwa moyoni mpaka huku nje na unajua chanzo ni uchungu. Na unataka upone kwenye maeneo hayo mawili yaani moyoni na mwilini. Cha kufanya hapo cha kwanza ni KUKITUMIA KINYWA CHAKO KUUNGAMA DHAMBI YAKO HIYO YA KUIFADHI UCHUNGU. Unajua watu wengi wanafikiri kuwa na uchungu moyoni ni haki yao kwasababu wameumizwa. Sikiliza  nikwambie huna haki wewe ya kuifadhi uchungu.

 

Ni kosa wewe kuhifadhi huzuni na hayo mauchungu uchungu. Ni sawa na mtu aliye na shamba likaotesha bangi hilo shamba na akaanza kuitunza hata kama haivuti. Siku ukishikwa huna haki ya kujitetea kuwa ilijiotea yenyewe afende!!! Utauluzwa swali hukuiona? Utajibu niliiona!! Watakuuliza hujui kuwa ni kosa kuwa na bangi? Utajibu ilijiotea yenyewe. Watakuambia kwani nini hukuitoa shambani kwako?

 

Hata kwenye eneo la dhambi ya uchungu ni hivyo hivyo. Huna haki ya kuiacha ikae kisa eti ulijeruhiwa ikaja yenyewe na ukaanza kuilea mpaka imekua kubwa weee na inatafuta kukuua. Mungu ili akuponye au akuhuishe hiyo nafsi yako ataanza kutafuta kinywani mwako unasema nini. Cha kwanza ni hicho UNGAMO LA MDOMO WAKO WEWE MWENYEWE. Ukifanya hivyo ndipo kinafuata kuombewa na hapo ndipo uponyaji hutokea.

 

Watu wengi dhambi imewajeruhi mno na wanatafuta kupona hawaponi kisa HAWAJUI NAMNA YA KUTUMIA KINYWA CHAO KWA KUIUNGAMIA AU KUITUBIA DHAMBI YAO ni  Kukubaliana na kosa na kulikiri kosa. Sasa watu wengi huficha maradhi yao ya moyoni na wanakufa kabisaa kiroho au  kimwili .

 

Uponyaji wa nafsi iliyoumizwa na dhambi upo kwenye mdomo wako wewe mwenyewe. Utamsikia mpendwa hapo ndiyo anaungama anaficha ficha dhambi wee. Anasema MIMI NI MWENYE DHAMBI NISAMEHE BABA!!! Dhambi ipi mpendwa? Nyoosha maelezo kwa ajiri ya afya ya moyo wako UNADHAMBI GANI?

 

Unapoungama au kutubu dhambi yako kwa kutumia kinywa chako, fahamu ndipo unapomfanya mponyaji mkuu Bwana Yesu Kristo akukaribie. Biblia inasema tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Ukitubu na kuziungama dhambi zako ndipo unapompa Mungu nafasi ya kuja kwako na kukusaidia.

 

Maandiko yanasema tunamshinda mshitaki wetu shetani kwa neno lile tunalolishuihudia. Neno unalolishuhudia litapitia kinywani. Umeona hapo. Ushindi wetu umo ulimini mwetu wala hauko mbali.

 

Sikia kama utajua namna ya kukitumia kinywa chako fahamu utafanikiwa sana kuwa na afya moyoni. Usifiche moyoni umivu lako liseme. Akikuumiza mtu sema mwambie huyo mtu au mwambie rafikio kuwa nimeumizwa na furani. Sikia. Unaposema ndiyo sehemu ya ufunguo wa  mlango  uliyokua unazibana fikra zako. Mtu anayesema kile kilicho moyoni mwake nakwambia ukweli afya ya moyo wake inakua nzuri kila wakati.

 

Hata watumishi. Kama umepewa moyoni mwako neno na neno hilo unatakiwa uliseme iwe kwa kufundisha au kuhubiri nk. Na ukayakalisha weee yakajaa huko ndani yako wala huyasemi Nakwambia tegemea MOTO HUKO UTAKAO KUCHOMA MPA MIFUPANI!!!! Msikilize Yeremia anasema hivi."Maana kila ninenapo napiga kelele, nalia, Dhuluma na uharibifu! Kwa kuwa neno la BWANA limefanywa shutumu kwangu, na dhihaka, mchana kutwa. Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia."(Yeremia  20:8-9).

 

Ndivyo ilivyohata kwa watu wengi sana. Wamejaza moyoni maneno ya Mungu mengi weeee!!! Hawataki kuyasema au kuwaambia wengine. Wengine wameacha kuhubiri au kufundisha nk. Sasa kwakuwa hawakisemi kile walitakiwa waseme MIOYO YAO HUPATA UGONJWA. Wakisema tu ndipo wanapopunguza ugonjwa.

 

Watu wengi wanatabia ya kukalisha mambo huko moyoni hawayatoi nje. Wanajikuta wamebeba mizingo mizito sana. Mungu alipokua anatuumba alijua hili. Ndiyo maana anatuinulia marafiki. Rafiki haletwi tu kwako ili akupe fedha nk. Analetwa pia kwako kama sehemu ya KUPUMULIA KWAKO KWA MAMBO YALEEE YAKUUMIZAO MOYONI.

 

Unajua unapokua na rafiki mwema,  unapoumizwa moyoni UKIMWAMBIA TU KUNA MZINGO UNAONDOKA HUMO MOYONI MWAKO. Sasa hapa ninataka uwe makini TAFUTA RAFIKI MWEMA KWA MUNGU. Kama Daudi na Yonathani.

 

Hata Bwana Yesu alikua na watu ambao aliwaita marafiki zake. Aliwaambia yaliyomo moyoni. Mfano alipopatwa na huzuni aliwaita Petro Yakobo na Yohana. Aliwaambia kuhuzu huzuni yake huko moyoni mwake. Mimi naamini hakuhitaji maombi tu ALIKUA ANAPUMUA!!! Nasema pumua na wewe ehehee!!!

 

Usikalishe mambo mengi moyoni utapasuka nakwambia jifunze kutumia kinywa kuaondoa yaliyomo humo moyoni, SEMA. Dhambi zikikuzidi usiziweke huko ndani zikajaa zitoe huku nje yaani  SEMA!!! Ukizisema fahamu ndiyo  unapumua moyoni nakwambia. KAMA HUNIELEWI NINAVYOSEMA SEMA NAMAANISHA UNGAMA WENGI WAMEZOEA KUSIKIA KUTUBU TUBU KWA KINYWA CHAKO PIA

 

Wewe wafuatilie watu waleee wampendao Mungu, na bahati mbaya wakatenda dhambi, na wakapata ujinga wa Kuificha moyoni hiyo dhambi bila kuisema au kuiungama kwa kinywa kwa marafiki.

 

Utaona wanatokewa na vitu viwili. Cha kwanza huvutwa kufanya dhambi nyingine. Kama alizini tu na akaficha. Utashangaa atafuatwa na wadada au wakaka wengi mno kuliko alivyokua zamani. Na usishangae ndiyo atazini na watu wengi mno.  Jambo la pili HUUGUA MNO MOYONI. Siku wakisema tu mimi naita kupumua UTASHANGAA FARAJA IMEKUJA MOYONI.

 

Dhambi isiyo tubiwa au kuiungama inaleta shida kweli  moyoni. Angalia mistari hii uone." Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha. Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako."(Isaya 38:16-17).

 

Huyu ndugu moyo wake ulipigwa, alitafuta kuhuishwa moyoni mwake na Mungu, unajua alikua nataabu kubwa moyoni iliyompelekea awe na huzuni. Huzuni hiyo ilizaa uchungu mkubwa moyoni. Unajua Mungu alimponya na kumuhuisha kabisaaa kwa kutumia ninini unajua?

 

Alimsamehe huyo mtu. Alipozitupa dhambi zake tu, huyo mtu akajikuta amepata amani moyoni na faraja na furaha. Kwa maana nzuri nafsi yake iliponywa. Angalia kitu hapo. Alipoondolewa dhambi moyo wake ukawa mzima.

 

Hata sasa Mungu anaweza kukutendea wewe hivyohivyo. TUMIA KINYWA CHAKO ILI UIPONYE NAFSI YAKO KWA KUUNGAMA DHAMBI ZAKO TU!! Angalia wapii umemkosea Mungu na umeficha? Ficha hiyo ndiyo inampa shetani nafsi ya kukukandamiza moyoni kwelikweli.

 

TUMIA KINYWA CHAKO KWA KUIKIRI KWA MUNGU NA KWA WATU ANASEMA NYINYI KWA NYINYI. Tafuta watu waaminifu wapo. Au rafiki mwaminifu yupo. Mweleze umebeba nini moyoni mwako vinavyokutesa. Iwe ni dhambi au gumu furani. Pumua au sema  mtu wa Mungu. Utaona uzima ukilejea taratibuuuu moyoni mwako.

 

Ebu tufuatane katika kipindi kijacho kwenye eneo hili la kutumia kinywa. Mungu akubariki sana.

 

Na: Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila.

admin