Skip to main content

MR & MRS MWAKATWILA | JIFUNZE NAMNA YA KUULINDA MOYO WAKO (AU NAFSI) NA KUUTOA KWENYE MAANGAMIZO Sehemu ya 1

62
0

Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana  ni imani yangu kuwa unaendelea vizuri na umekua na shauku ya kupokea somo darasani. Namshukuru Mungu ambaye ameendelea kutulinda na kutupigania.  Pia nashukuru sana kwa maombi yako kwa ajili ya kupewa somo jipya darasani. Leo hii tunaanza kujifunza somo jipya na zuri na refu kidogo darasani.

Nilipokua namuomba Mungu anipe somo la wakati, Mungu ametupa somo lenye kichwa hiki.

JIFUNZE NAMNA YA KUULINDA MOYO  WAKO (AU NAFSI) NA KUUTOA KWENYE MAANGAMIZO.

Ebu tuanze kujifunza taratibu mpaka Roho Mtakatifu atakapo tuweka mwisho katika somo hili. Sikiliza. Ukiyasoma maandiko matakatifu yaani Biblia, humo ndani utakutana na maagizo mengi sana ambayo Mungu ametuagiza tuyafanye. Na moja ya agizo muhimu sana ambalo mimi na wewe tumepewa tulifanye ni hili la kuulinda moyo au nafsi yako.

Angalia mistari hii ambayo ndiyo imebeba ujumbe mzima wa somo hili. Mandiko yanasema hivi. " Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.  Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima."(Mithali 4:20-23).

Ukiisoma mistari hiyo utaona Mungu anatuimiza mimi na wewe tuhakikishe tunazisikia kauli zake. Anasema kauli zake ndani yake zimebeba uhai kwa wale wasipatao au wazisikiazo  na afya mwilini. Na ndani ya kauli yake anatoa agizo kwa kila mtu atakae uhai na afya ahakikishe anaulinda sana moyo wake kuliko vitu vyote avilindavyo.

Kabla sijasogea huko mbele nilitaka nikujulishe kuwa moyo unaotajwa hapo si moyo huu wa nyama. Moyo unaotajwa hapo ni nafsi. Neno nafsi kwa lugha nyingine ndani ya maandiko unaitwa moyo. Ngoja nikupe mifano hii michache naamini utaelewa hiki ninachokufundisha."Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu."Kum 10:16)

Angalia na mstari huu. " Jitahirini kwa BWANA, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu"(Yetemia 4:4)

Sikiliza, Biblia inavyosema moyo utahiriwe hazungumzii moyo huu wa nyama unaosukuma damu. Kama angekua anataka moyo huu wa nyama usukumao damu utahiliwe mimi nakwambia WATU WENGI WANGEKUFA. Unautahilije moyo huu wa nyama? Ehehee.nimekupa neno makusudi ili ujue ni moyo upi unaotakiwa utahiriwe. Nenda kamtafute daktari yoyote yule leo mwambie aisee!! Nimekuja naomba uutahiri moyo wangu? Eheheee

Watu wengi wakisikia neno itakaseni mioyo yenu wengi hufikiri moyo huu unaodundadunda kifuani. Sikia si moyo huo unaotajwa . Ebu itazame hii mistari uone ninachokuambia .  " Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi."(Mambo ya Walawi 17:11).

Ukiisoma mistari mingine utaona upatanisho huo wa damu hiyo unatajwa kuwa ni moyo wa mtundiyo unaopatanishwa na Mungu.  hapo kuna neno nafsi kutakaswa kwa damu, sasa usipojua unaweza fikiri anazungumzia vitu viwili tofauti. Maandiko yasemapo takasa nafsi  kwa maana nyingine anakuambia takasa moyo. Tumeumbwa na Mungu katika sehemu kuu tatu. Roho au mtu, Nafsi au moyo kwa neno lingine inaitwa pumzi hai ya Mungu na mwili au mavumbi.

 Angalia mistari hii uone." Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba."(Mwanzo 1:27). Mungu aliumba mtu kwa mfano wake, na maandiko yanatufundisha kuwa Mungu ni Roho. Bwana Yesu anatufundisha hivi. " Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."(Yohana 4:24). Anaposema aliumba mtu kwa mfano wake maana yake aliumba roho. Kwahiyo neno mtu linasimama badara ya neno roho.

Alipofanya uumbaji ule wa kwanza wa kuumba mtu yaani roho, Mungu  akamuongezea huyo mtu vitu vingine viwili yaani mwili au mavumbi na nafsi au moyo au pumzi hai ya Mungu. Angalia mistari hii. Inavyotufundisha" BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."(Mwanzo 2:7). Ukiisoma hiyo mistari utagundua kuwa mtu alipewa kitu cha pili kinaitwa mavumbi au mwili huu ulio na damu nyama mifupa mishipa na maji na ngozi nk. Sasa ukijifunza elimu hiyo utaona Mungu alituumba sisi kwa kutumia hizo sehemu tatu. Yaani roho nafsi na mwili.

Ngoja nikuonyeshe jambo lingine naamini utaelewa zaidi. Angalia na mistari hii tena ukione kitu hiki. " Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama."(Ezekiel 36:24-26).

Moyo wa jiwe au moyo mgumu unaweza kulainishwa au kuhuishwa ukawa laini kama nyama. anaposema atakupa moyo wa nyama maana yake atakupa moyo au nafsi ILIYOPONDEKA!!! Haujawahi sikia neno hili, watu hawa wana moyo mgumu? Au neno msiifanye mioyo yenu kuwa migumu? Ukisikia neno hilo kinachosemwa ni nafsi.  Naamini sasa unanielewa ninaposema neno moyo naneno nafsi ni kitu kimoja.

Sasa sikia, Mungu amekupa agizo wewe la kuulinda huo moyo wako. Bahati mbaya  sana watoto wa Mungu wengi kwenye eneo hili hawawajibiki wao kama ipasavyo katika kuhakikisha wanazilinda  hizo nafsi zao kama Mungu alivyotuagiza. Watoto wa Mungu wengi sana utawasikia wanasema Mungu linda moyo wangu. Na Mungu nayeye atakuleta kwenye mstari huo. Atakwambia mwanangu linda moyo wako kuliko vitu vyote uvilindavyo!!!!

Unaweza kupata swali kama hili moyoni mwako je! Mungu yeye hazilindi nafsi zetu? Jibu ni rahisi tu. anazilinda sana. Msikilize asemavyo katika maandiko matakatifu. "Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele."(Zaburi 121:1-8)

Ukiisoma mistari hiyo utaona Mungu yupo tayari kutulinda sisi na mabaya yote, pia atazilinda nafsi au mioyo yetu. Hapo unaweza kupata swali lingine, kama Mungu yupo tayari kuzilinda hizo nafsi zetu kwanini atuagize sisi tuzilinde? Inakuaje tena atuagize sisi tulinde mioyo yetu tena tulinde kuliko vitu vyote?

Sikiliza, Mungu kweli ni mlinzi wetu, na ili akulinde moyoni mwako kuna maagizo maalumu ambayo yeye atakupa wewe uyafanye ili KUUTIMIZA ULINZI WAKE KWAKO. Hata anapotupa sisi wajibu wa kulinda mioyo yetu ameanza kwa kusema hivi. " Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.  Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima."(Mithali 4:20-23).

Fahamu ndani ya kauli yake kuna utaratibu furani ameuweka ili wewe uufuate. Unapoufuata ndipo ulinzi wake kwako unakua mkubwa. Kwa maana hiyo. Mungu ni mlinzi wa moyo wako na wewe unawajibu wa kuulinda moyo wako kwa kufuata utaratibu atakaokupatia. Kama hauufuati fahamu hawezi kukulinda moyoni mwako nakwambia. Sikiliza nikwambie, Mungu ili afanye jambo lolote kwako fahamu kuna utaratibu maalumu atakupa ili alifanye hilo alilolikusudia kulifanya kwako.

Ngoja nikupe mfano huu utanielewa. Mungu ili awalinde wana wa Israeli na muharibu siku ile kule Misri. Aliwapa utaratibu wa kupaka damu milangoni mwa nyumba zao kwenye kizingiti na miimo yake. Jiulize hivi siku ile kama kuna mtu angeenda kinyume na utaratibu ule ingekuaje? Nakuhakikishia mtu huyo nayeye yangemkuta yaliyowakuta Wamisri yaani kufiwa na wazaliwa wa kwanza.

Umewahi jiuliza swali hivi siku ile Mungu anataka kuwalinda wana wa Israeli dhidi ya jeshi la Farao lilipo wafuata baada ya kutoka Misri kwa kumpa Musa utaratibu wa kuiinua fimbo juu ya maji ya  bahari ya Shamu ingetokea nini kama Musa asingelitii agizo lile? Jibu ni rahisi tu wangeshikwa na kuludishwa utumwani.

Ni sawa na leo hii Mungu ili akulinde wewe na usiingie jela ya milele yaani jehanamu amekupa utaratibu huu MWAMINI BWANA YESU KRISTO PIA TUBU USIFICHE DHAMBI ZAKO. Wewe hutaki kuufuata utaratibu huo unafikiri jibu lake nini? UTAUKOSA ULINZI HUO SIKU HIYO INAKUJA. Utakwenda jehanamu.

Ngoja nikwambie neno. Siku moja kwa neema yake Mungu , alinionyesha jehanamu ilivyo. Nilipata neema hiyo ya kuonyeshwa jehanamu. YAANI WAPENDWA USIOMBEE UENDE HUKO. Jehanamu ipo. Sikuona mtu ndani ya LIMOTO LILE.

 Lakini mimi mwenyewe niliona tu  sikuingizwa mle ndani lakini  NILITETEMEKA SANA. MPAKA LEO HII NIKIKUMBUKA NAOGOPA. Nakumbuka Bwana  aliniambia nilipomwambia SITAKI KWENDA KWENYE MOTO HUO SIKUA ALITAKA KUNIINGIZA MOTONI. ILA NILISEMA MIMI HUKU NIKITETEMEKA SANA . Unajua alinijibuje?  ALINIAMBIA HIVI LUDI NENDA UKAWAAMBIE WATU WASIJE KUINGIA MAHALI HAPO!!

Ngoja leo hii niseme neno hili nauhakika nalo kabisaa. Nakuhakikishia Mungu hapendi wala hafurahii kuona mtu anakwenda jehanamu. Na ili tusiende huko katupa utaratibu. Maandiko yanasema  hivi." Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao. Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu."Yohana 5:21-29).

Ukiyaangalia maneno hayo utaona Mungu ameweka utaratibu wa kila mtu atakaye siku ile awena uzima afanye nini leo. Kama hauufuati utaratibu huu unafikiri kwako kitatokea nini siku ile? Unajua ninajaribu kukuonyesha Mungu alivyo anatabia ya kuweka utaratibu. Ili akulinde wewe na huo moyo wako kakuambia nawewe ulinde. Kwa lugha nzuri lindo la moyo wa mtu litategemea mtu mwenyewe kaamua kulilindaje. Neno linda maana yake kuna adui anaweza kushambulia.

 Pia Mungu hawezi kukuambia linda moyo wako kama wewe huwezi linda. Mungu anajua kabisa kuwa mtu anaweza kulinda moyo wake. Unajua Neno la Mungu linavyouzungumzia moyo linauzungumzia kwa namna nyingi sana. Angalia maneno haya." BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao."(Kutoka 4:21).

Mungu hapo aliufanya yeye moyo wa Farao kuwa mgumu. Sasa angalia mistari hii uone kitu." Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,"Waebrania 3:8).

Ukiisoma hiyo mistari yote yaani ule wa kitabu cha Kutoka na huu wa Waebrania. Utaona Mungu anao uwezo katika moyo wa mtu kuufanya mgumu na mtu anao uwezo yeye mwenyewe kuufanya moyo wake kuwa mgumu. MUNGU ANAWEZA KUFANYA JAMBO KWENYE MOYO WAKO NA WEWE UNAWEZA KUFANYA JAMBO KWENYE MOYO WAKO.

Sasa anapokupa wajibu wewe wa kuulinda moyo wako fahamu unayonafasi furani wewe ya kuufanya moyo wako kupokea ulinzi kutoka kwa Mungu na ndiyo maana anakuagiza wewe LINDA MOYO WAKO KULIKO VITU VYOTE ULINDAVYO.

Naamini umenielewa, ebu fuatana nasi katika kipindi kijacho ili tujifunze tena kwa upana somo hili.

Mungu akubariki sana.

Wako

Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwil

 

 

admin